Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anunua hisa katika mtandao wa simu za mkononi ya Vodacom
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema amenunua hisa za kampuni ya Vodacom
Tanzania Plc zenye thamani ya shilingi milioni 10 pamoja na nyingine za
shilingi milioni 10 kwa ajili ya mke wake, Mary Majaliwa.
Alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari mbele ya wakuu wa masoko ya Hisa na Dhamana, Soko la Hisa la Dar es Salaam, viongozi wa Baraza la Uwezeshaji na Kampuni ya Vodacom katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kueleza alichofanya, Waziri Mkuu aliwasihi Watanzania walioko ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kununua hisa hizo ili waweze kuwa wamiliki wa kampuni kupitia hisa zao.
Alisema anajua watumishi wa umma wamepewa fursa ya kununua hisa hizo kupitia mipango iliyowekwa na Makatibu Wakuu wao, lakini pia amewasihi viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi wachangamkie fursa hiyo ili nchi iweze kupata kodi kupitia makampuni hayo.
Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema uwekezaji kwenye hisa ni njia mojawapo ya kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa nchi.
Waziri Mpango alisema anatoa ombi maalumu kwa wafugaji kukubali kuuza mifugo yao na kununua hisa ili kupunguza idadi ya mifugo yao na kupunguza misuguano baina yao na wakulima.
Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao alisema mauzo ya hisa yanayofanywa na kampuni hiyo ni makubwa mara nne ya mauzo ambayo yamewahi kufanyika hapa nchini. Alisema kampuni hiyo ambayo imekwishafanya kazi kwa miaka 17 hapa nchini, imewekeza zaidi ya Sh trilioni mbili katika mtandao wa mawasiliano nchini Tanzania.

Comments
Post a Comment