Makala - Baadhi ya hadha wanazo zipata wanafunzi katika suala zima la usafiri



HADHAWANAYOIPATA WANAFUNZI KATIKA SUALA ZIMA LA  USAFIRI
WAKATI mikakati mbalimbali ya kuongeza kiwango cha elimu kwa wanafunzi ikiendelea kufanyiwa kazi, bado kuna changamoto ya usafiri wa uhakika kwa wanafunzi haujaangaliwa kwa jicho la umakini.
Inawezekana likaonekana suala la kawaida kwa sababu limepigiwa kelele kwa muda mrefu, lakini mwanafunzi anahitaji kuwa na utulivu wa akili anapoamka na anaporudi nyumbani kutoka shule.
Leo katika makala hii tunakwenda kuangazia hadha wanayo ipata wanafunzi katika suala zima la usafiri, ili kujua hayo na mengine mengi ungana name Juma K Juma
 Yote yanakamilika kwa kupata nyenzo nzuri ya kumpeleka shule asubuhi na kumrudisha nyumbani jioni.
“Changamoto zipo kwa wanafunzi wa shule za Kata, lakini kwangu nashukuru kwani ninaweza kuwahi masomo yangu na kurudi nyumbani kwa wakati; hivyo nayamudu masomo yangu bila changamoto ya usafiri,” anasema Zamda Chacha
Tafsiri ya maelezo ya mwanafunzi huyu ni kuwa shule za binafsi mara nyingi zipo katika mikono salama kutokana na utaratibu wa kuingiza usafiri katika malipo, hawafikirii kugombania usafiri vituoni wala kugombana na makondakta kutokana na kiasi kidogo cha nauli wanacholipa.
 Manyanyaso ya wanafunzi kutokana na kiasi kidogo cha nauli walichopangiwa na serikali kinawakera makondakta na madereva, Sh 200 wanayolipa inawakosesha ruhusa ya kukaa kwenye viti au ikiwa gari halijajaa wanalazimika wasubiri hadi lijae ndio waruhusiwe.
 hiyo inawakatisha taama wanafunzi wengi na wanafunzi wa kike wengine wanajiingiza katika mapenzi ya mapema ili wapewe lifti, hayo ni maisha hatarishi na tabia mbaya
.” Hivyo inaonyesha ni jinsi gani usafiri inavyokwamisha kiwango cha ufulu kwa wanafunzi, na kukatisha malengo yao waliyojiwekea.
 “Suala la wanafunzi kuchelewa linatuweka katika wakati mgumu, mara nyingine mwalimu anaacha zoezi ubaoni lakini kesho ukija unakuta mwanafunzi hajafanya na ukimuuliza anasema nilichelewa kufika shule kwa sababu ya usafiri kama mwalimu nalazimika kurudia mada iliyopita, ” anasema Mwalimu Abeid Issa
            Na kwa kuendelea pia nimepata nafasi ya kumuhoji konda mmoja wa magari yanayo elekea kihonda  na mjini naye alikua na haya yakuongea “wanafunzi hawapati shida sana katika mabasi yao ya kihonda lakini kila siku zinapozidi kusonga mbele itawabidi wanafunzi wasimame kwa wakati mwingine na kwa upande wa wao wanatoa pesa kidogo ambayo ni shilingi 200/=tsh” alisema konda Mkali
 Aidha, wanafunzi wanaosoma shule za mbali ndio wanaoumia sana kwa sababu wanakaa njiani kwa zaidi ya saa tatu kuenda na kurudi shule. Inawezekana wanatumia muda mwingi barabarani kuliko muda wanaoutumia shule au nyumbani.  
Tatizo hili haliathiri wanafunzi tu bali hata walimu kama alivyosema Mwalimu Abeid ambaye hulazimika kurudia somo mara kadhaa ili hata wale wanafunzi waliochelewa wapate kujua nini kilifundishwa.
 “Kungekuwa na usafiri kwa wanafunzi ingekuwa afadhali, kama wazazi tungechangia tu kama tunavyachangia chakula kwa wanafunzi shuleni ili kuokoa elimu ya watoto wetu isishuke”Amesema mzazi.
Ukweli utabaki pale pale kama kweli tuna nia ya dhati ya kuongeza ubora wa elimu wanayoipata wanafunzi hapa nchini basi ni lazima mazingira rafiki yatengenezwe ili mwanafunzi asikutane na changamoto kama hizo zinazokatisha tamaa.
 Uongozi wa shule kwa kushirikiana na wazazi wanaweza kutatua taizo hilo, pia serikali inaweza ikaweka mkono wake katika usafiri wa umma kwa kuwa mbali na nauli kushushwa lakini bado nafasi ya kupata usafiri kwa wanafunzi inakuwa ngumu kwani huambulia manyanyaso kutoka kwa makondakta wa usafiri huo.
Mwisho wa makala hi indo mwasho wa makala nyingine nzuri.
Na mwandishi wetu.

Comments

Popular posts from this blog

Makala - Historia ya Hip Hop Tanzania

Makala - Kilimo cha Mboga Mboga