Makala - Kilimo cha Mboga Mboga

Mti wa Bilinganya


UANDAAJI WA KILIMO CHA MBOGA MBOGA


Kilimo ni hazina katika nchi yoyoe mali hiyo ina manufaa kwa mtu binafsi na   kwa taifa kwa  ujumla.Nchi yetu ya Tanzania ina kilimo cha aina nyingi ,baadhi ya vilimo hivyo ni vya mboga mboga na matunda  na chakula.
            Hii leo tunakuletea kilimo cha  mboga mboga hasa tunaangazia zaidi kilimo cha  mchicha,kabichi na Chinese ambavyo ndivyo vinatajwa nqa wtu wengi kuwa ndiyo mboga maarufu na inzaalishwa kwa wingi  katika nchi ya Tanzania.
Tunaanza na zao la mchicha,Mchicha ni zao ambalo  hulimwa kwa wingi sehemu yenye udongo wa ufinyanzi na utifutifu kwa mkoa wetu  wa Morogoro hasa Morogoro mjini zao la mchicha hulimwa sana maeneo ya mji mpya,kichangani na maeneo mengine ambayo yamepitiwa na mito au sehemu nyingine zenye maji mengi.
Mchicha umegawanyika katika sehemu kuu mbili nazo  ni mchicha wa asili na mchicha wa kupandwa,Mchicha wa asili ni ule ambao umeota bila kupandwa na mwanadamu ambao jina lake maarufu huitwa mchicha bwasi na mchicha uliopandwa na mwanadamu umegawanyika katika makundi tofauti upo unaoota baada ya siku saba na siku tano.
Mchicha ambao majani au maua yake hutumika kama chakula hutibu magonjwa yafuatayo kuuma mgongo,unatibu figo,tezi shingo,kusafisha njia ya mkojo,kusafisha damu,dawa ya kikohozi na inasaidia kupata haja kubwa kwa wingi .
Msomaji wa makala hii nakushauri sana utumie mboga hii ya mchicha kwa ajili ya kuimarisha afya yako ili uweze kuwa mtu makini katika taifa hili,pia tutunze vizuri ardhi yetu na vyanzo vya maji kwa ajili ya kuweza kustawisha mboga zilizo bora kwa manufaa ya watu walio sasa na baadae hiko ndicho kilimo cha mchicha hiyo ndiyo mboga bora  kwa mwanadamu.
Kabichi ni zao ambalo ustqawi zaidi katika mikoa ya  Arusha,Kilimanjaro,Morogoro,Tanga,Iringa na Mbeya.kabichi ina madini aina ya chokaa,protini na maji kwa wingi ,mboga hii inaweza kuliwa bila kupikwa au kuchemshwa kwa kutengenezwa kachumbari pia inaweza kupikwa pamoja na vyakula kama vile mahargwe na nyama.
Kabichi ni zao ambalo upendelea zaidi hali ya baridi zao hili hustawi  na kutoa mazao mengi na bora zaidi  kwenye sehemu zenye miinuko ya kuanzia mita 1200 hadi 1900 kutoka usawa wa bahari zao hili ustawi zaidi katika udongo wa kitifutifu na wenye rutuba nyingi na uwezo wa kuhifadhi unyevu kwa muda mwingi vilevile linaweza kustawi katika aina mbalimbali za udongo ilimradi udongo huo usitwamishe maji na usiwe na chumvi nyingi.
Endapo udongo hauna rutuba ya kutosha uongezewe mbolea za asili kama mbolea ya samadi na vunde,kabichi zinazolimwa hapa Tanzania ni prize druntied ambayo vichwa vyake ni vikubwa kilo 2 mpaka kilo 2 na nusu na ni bapa ambayo huchelewa kukomaa siku 110 hadi 120 tangu kupandikiza miche na hupasuka kirahisi aina hii huvumilia hali jua kali
Copenhagen market,vichwa vyake ni vya mviringo na hupasuka kirahisi aina hii pia hukomaa mapema siku 90 hadi 100 tangu kupandikiza miche
Groly of enkhiuzen,vichwa vyake ni vya mviringo hii huvumilia hali ya jua kali lakini huchelewa kukomaa siku 100 hadi 120 tangu kupandikiza miche na havumilii hali ya kupasuka.Aina nyingine ni Brunswick na Danish ball head.
Kabichi ni zao linalotumia virutubisho vingi aridhini kulinganisha na mboga zingine.Hivyo kabla ya kustawisha panda mazao jamii ya mikunde ili kuongeza rutuba,Halikadhalika baada ya kuvuna panda mazao yanayotumia chakula kidogo kama vile karoti hubadilisha mazao pia hupunguza kuenea kwa wadudud waharibifu na magonjwa.
Mbegu za kabichi huanza kuoteshwa kitaluni na baadae miche huamishiwa shambani ,lima vizuri sehemu itakayooteshwa mbegu,weka mboleaza asili zlizooza vizuri kiasi cha ndoo 5 hadi 10 zenye ujazo wa lita 20 kwa eneo la mita mraba 10.Changanya vizuri mbolea na udongo kasha lainisha udongo kwa kutumia reki.Baada kulainisha udongo tengeneza tuta lenye nafasi ya sentimita 10 mpaka 15 kutoka mstari hadi mstari.
Funika mbegu kwa udongo au mbolea laini kasha tandaza nyasi kavu ili kuhifadhi unyevu,mwagilia maji kila siku asubuhi na jioni mpaka mbegu zitakapoota ,miche huwa tayari kwa kupandikizwa shambani baada ya majuma 3 hadi 5 tangu kuoteshwa.
Kabichi hukomaa na kuvunwa baada ya siku 60 hadi 120 kutegemea aina iliyostawishwa tangu kupandikizwa miche.
Chinese ni moja kati ya mazao ya mboga mboga inayolimwa sana nchi Tanzania,asili yake ni China na baadae ikasambaa dunia nzima.Chinese inakuwa vizuri kwenye jotolidi 18 hadi 22,zao hili linategemea maji mengi wakati wa ukuaji na linakua vizuri kwenye udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha,wakati unaandaa shamba udongo utifuliwe vizuri kabla ya kupanda na andaa shamba wiki 6 kabla ya kupanda .
Jinsi ya kuandaa kitalu kinatakiwa kiwe na upana wa mita 1 na urefu wa mita 5.Kitalu kinatakiwa kiwe na kingo ili kuzuia maji kutoka nje ya kitalu kasha panda mbegu kwenye kitalu kwa sentimita 15 hadi 20 mstari hadi mstari.
Tumia mbolea ya kuku,mbuzi na nguruwe,tumia ndoo katika kila kitalu chenye mita 5 na pia weka mbolea ya
            Kukuzia ya UREA kwa kila kitalu pale mmea unapofikia majani 5.Chinese hukoo baada ya miezi  3 hadi 4 inategemea na aina.Vuna kwa kutumia kisu au mkono,maisha ya Chinese ni mafupi sana tofauti na mboga zingine,hivyo unatakiwa kusafisha na pia baada hapo unaweza kutunza kwenye friji ili kuzuia kukauka.na hizo ndizo mboga mboga zinazosababisha mwanadamu kukua vizuri bila kupatwa na magonjwa.
 



Mboga aina ya kabichi

Comments

Popular posts from this blog

Makala - Historia ya Hip Hop Tanzania