Kitu ambacho watakiwa kukifanya endapo utahisi siku yako haiko poa



 Unaamini kabisa kwamba siyo siku zote huwa zinafanana. Mara nyingine siku huanza vema na kuendelea kwa furaha amani na mafanikio hadi mwisho wa siku hiyo.

Mara nyingine siku yako huanza vibaya na kuishia vizuri, lakini ziko siku ambazo huonekana kuanza kwa mabalaa kama vile bahati mbaya, kupoteza vitu, kuumia, au huzuni ya moyoni na wengine hutabiri muonekano wa siku nzima kuanzia kwa yale yaliyojiri asubuhi. Watasha wamesema: “siku njema, huonekana asubuhi” maana yake, mara nyingine hata siku mbaya pia hujionyesha katika mwanzo wa siku hiyo.

Najua kuna baadhi ya imani zisizo rasmi ambazo hujaribu kulielezea suala hili. Mfano; Ukiona bundi asubuhi au ukipishana na vyoka njiani basi kuna walakini na siku yako hiyo. Wapo wengine hasa wazungu ambao husema : “ameamkia upande mbaya wa kitanda” sina uhakika kama kuna upande mbaya na mzuri wa kitanda. Nia yangu ni kujaribu kukupa namna za kitaalamu zinazoweza kukusaidia kuigeuza siku yako iliyoonekana kuanza vibaya kuwa nzuri na kupunguza pia uwezekano wa kuwepo kwa hizi siku zinazoaminiwa kuwa mbaya.

Mambo ya kuzingatia:
Jikubali kama mwanadamu wa kawaida na kwamba haistajabishi kushindwa
Yamkini unakata tamaa maana umezungumza na watu wanaoshinda na kufanikiwa tu, angalia upande wa pili, zungumza pia na waliowahi kushindwa.
Haijalishi ni muda gani, ni kiasi gani, ni ukubwa gani, ni uzito kiasi gani, wa magumu uliyopitia ninachojua ni kwamba inawezekana mimi na wewe kunyanyuka tena toka kushindwa kwetu, ndoto zetu zaweza kuwa kweli tena. Hii inategemea na kiasi cha uvumilivu wako.

Tatizo siyo kushindwa. Kushindwa kwa ukweli ni kule kushidwa kunyanyuka tena mara baada ya kushindwa mara ya kwanza
Angalia mchezo wa ngumi, haijalishi mtu anapigwa na kuanguka mara nyingi kiasi gani, lakini pale anaposhindwa kunyanyuka ndiyo refa hutangaza “KNOCK OUT” yaani ameshindwa kabisa.

Ili kuweza kunyanyuka tena;
Jikubali kama mwanadamu wa kawaida tambua kushindwa kupo na ni moja ya matukio ya maisha yetu.
Unapoanguka chini, jitahidi usibaki chini. (Tofautisha kuanguka kwa mtoto na mtu mzima) fahamu kushindwa kwa kweli ni kule kushindwa kunyanyuka mara baada ya kuanguka.

Jifunze, pata shule kupitia mapito na magumu unayoyapitia, tatizo pia siyo kufeli, bali ni kufeli kujifunza katika kule kufeli. Kufanye kushindwa kwako kuwe kama mawe ya kukanyagia katika kuvukia kwenda upande wa pili.
Jitahidi sana kufanya ibada nakumuomba Mungu kwasababu yeye ndio kila kwetu na ameahidi kuwa atakae muomba ata mjibu dua yake

Comments

Popular posts from this blog

Makala - Historia ya Hip Hop Tanzania

Makala - Kilimo cha Mboga Mboga