Bongo Flava ni jina badala la muziki wa Hip hop ya Tanzania. Mtindo huu ulianzishwa kwenye miaka ya 1990, hasa ukiwa kama mwigo au utokanaji wa hip hop kutoka Marekani, ikiwa na ongezeko la athira ya muziki wa reggae, R&B, afrobeat, dancehall, na mitindo ya asili ya Kitanzania kama vile taarab na dansi, muunganiko ambao umeunda mtindo wa pekee wa muziki Mashairi kawaida huwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Jina la "bongo flava" ni tokeo la matini yaliyoharibiwa kutoka "bongo flavour", ambapo "bongo" ni wingi wa neno ubongo ambapo mara nyingi huchukua nafasi ya kutaja jina la utani la Dar es Salaam, jiji ambalo mtindo aina ya mtindo huu inatokea. Katika bongo flava, sitiari ya "bongo" inaweza kutaja zaidi maana ya ujanjaujanja wa mtaani, ya msela au masela wingi wake. Istilahi ya "bongo flava" ilitajwa kwa mara ya kwanza mnamo 1996 na Radio One 99.6 FM (moja kati ya redio za kwanza kabisa za binafsi nchini Tanzani...