MAKALA - USIYOYAJUA KUHUSU UGONJWA WA MATENDE
USIYOYAJUA KUHUSU UGONJWA WA MATENDE Ugonjwa wa matende ni aina ya ugonjwa unaosababisha ngozi na tishu zilizo chini ya ngozi ya mwanadamu kuwa nene (thickening of skin and underlying tissue).Ugonjwa huu huathiri miguu,mikono, figo, korodani na kusababisha korodani kuvimba na kuwa kubwa sana. Inakisiwa watu milioni 120 duniani wana maambukizi ya ugonjwa huu ambapo kati yao milioni 40 wamepata madhara makubwa kutokana na ugonjwa huu. Kati ya hawa walioathirika theluthi moja huapatikana katika bara la Afrika, theluthi moja nyingine hupatikana India,na kiwango kilichobakia hupatikana katika visiwa vya Pacific, Marekani na Asia ya kusini. Aina nyingine ya ugonjwa wa matende inayojulikana kama nonparasitic elephantiasis au podoconiosis ambayo haisababishwi na vimelea vyovyote hupatikana katika nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda,Burundi) Sudan, Egypt na Ethiopia.Asilimia 6 ya maambukizi ya aina hii ya podoconiosis hupatikana nchini Ethiopia. Nini...